Dk Mwinyi afanya mabadiliko ya viongozi Wizara ya Katiba

Unguja. Rais wa Zanzibar,  Dk Hussein Mwinyi amefanya mabadiliko ya wakurugenzi watatu katika Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Juni 12, 2024 ikiwa imesainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Zena Said imemtaja Bakar Khamis Muhidin kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali watu.

Awali alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya uendeshaji na utumishi.

Maulid Shaib Ahmada ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya miundo ya taasisi, utumishi na maslahi ya watumishi. Kabla ya hapo alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mipango ya Rasilimali watu.

“Ndugu Yussuf Moh’d Suleiman ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya uendeshaji na utumishi, kabla ya uteuzi huo alikuwa Ofisa Mwandamizi katika Idara ya miundo ya taasisi, Utumishi na maslahi ya watumishi,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Related Posts