Waagizaji wa mafuta nchin waondolewa hofu juu ya ukarabati wa boya la kushushia mafuta ya nishati aina ya dizel

Mkurugenzi wa bandari ya Dar es salaam , Mrisho mrisho amewaondoa hofu waagizaji wa mafuta nchini kuwa ukarabati utakaofanyika katika boya la kushushia mafuta ya nishati aina ya dizel baharini kupitia bomba la tazama hautakuwa na athari katika ushushaji wa mafuta.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam baada ya kutembelea eneo la kushusha mafuta ya baharini na meli zinaxoshusha mafuta ni zebye uwezo wa kabeba zaidi ya tani laki moja za mafuta

Mkurugenzi Mrisho amesema Kukosekana kwa miundombinu ya kuhudumia meli hizo katika bandari ya Dar es salaam boya hilo hitumika kuhudumia meli hizo ambapo kila baada ya kuhudumia wastani wa meli moja bomba za kupakua mafuta hutakiwa kufanyiwa matengenezo, akaongeza kuwa wakati ukarabati ukifanyika katika bomba la TAZAMA, bomba lingine lenye ukubwa wa kipenyo cha inchi 24 litatumika kuhudumia meli hizo

Ukarabati huo utahusisha kubadilisha bomba zinazopakua mafuta kutoka kwenye meli hadi kwenye hifadhi za mafuta zilizopo kigamboni (floating horze ) na unataraji kutafanyika kwa siku saba kuanzia juni 21 – mpaka 27

Hivi karibuni Mamlaka ya usimamizi wa bandari TPA ili saini mkataba wa ujenzi wa terminal ya kupokelea mafuta katika bandari ya dar es salaam unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 600ili kuwezesha meli kubwa za mafuta kuhudumiwa.

Related Posts