Waandishi toeni taarifa sahihi juu ya zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura nchini

Kuelekea zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura nchini itakayo anza julai misi maka huy waaandishi wa habari wametakiwa kutumia majukwaa yao kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha kuwa wapiga kura, Pamoja na kuboresha taarifa zao katika Daftari hilo ili waweze kupiga kura na kuchagua viongozi wanaowataka.

Akizungumza  jijini Dar es Salaam katika mkutano mahususi wa uchaguzi   Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ulioikutanisha Tume Huru ya Uchaguzi (INEC,) na na waandishi wa habari wapatao 250,Katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Huduma za Utangazaji kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka amesema, waandishi wa habari wamekuwa nyenzo muhimu ya upatikanaji wa tarifa kwa wananchi kupitia vyombo vya habari  hivyo zina wajibu wa kushirikiana  na Tume kwa ukaribu zaidi hususani katika wakati wa kabla na kipindi cha uchaguzi.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (Maelezo), Bw. Patrick Kipangula akiwasilisha mada kuhusu maadili ya uandishi wa habari hasa wakati wa uchaguzi amesisitiza kuwa Tume inatarajia kupata ushirikiano mkubwa zaidi kutoka kwa waandishi ,ambapo amewataka kuzingatia sheria, kanuni, miongozo, taratibu na maelekezo wakati wa kuwafikishia wananchi taarifa sahihi na kwa wakati zinazohusu zoezi  la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura


Kwa mujibu wa Kifungu cha 16 (5) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024, Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utakuwa mara mbili kati ya kipindi kinachoanza mara baada ya uchaguzi mkuu na kabla ya siku ya uteuzi. na wanaohusika katika zoezi hili ni wananchi ambao: –

1.Wametimiza umri wa miaka 18 na kuendelea ambao hawakuandikishwa hapo awali;
2.Watakaotimiza miaka 18 kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025;
3.Waliojiandikisha awali na wamehama Kata au Jimbo moja kwenda jingine;
4.Waliopoteza sifa mfano wale waliofariki kuondolewa katika Daftari;
5.Wenye taarifa zilizokosewa wakati wa uandikishaji; na
6.Waliopoteza au kadi zao kuharibika.

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)pia  imetoa wito kwa waandishi wote wa habari kutumia majukwaa, taasisi na mashirika yao kuhamasishana kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Mkutano huo ambao ni mwendelezo wa vikao vya wadau vilivyoanza Juni  07, 2024 ulikuwa na lengo la kuwapa wadau hao wa uchaguzi taarifa mbalimbali za maandalizi kwa ajili ya kuanza rasmi kwa zoezi la uboreshaji wa Daftari.

Related Posts