BEKI wa kati wa Simba, Henock Inonga ambaye awali alikuwa anatajwa kutua FAR Rabat ya Morocco huenda dili hilo likafa baada ya klabu ya FC Metz inayoshiriki Ligi 2 ya Ufaransa kuingilia kati na kumtaka.
Inaelezwa kuwa, dili la beki huyo kutoka DR Congo kwenda FAR Rabat limeota mbawa baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Nasreddine Nabia aliyekuwa anamhitaji anajiandaa kutua Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini. Inonga ambaye hajatumika katika mechi kadhaa za mwishoni mwa msimu kwa kilichoelezwa kuwa majeruhi, japo taarifa nyingine zinasema ni ‘mgomo’ baridi aliokuwanao kutokana na kutuhumiwa tangu pambano la Dabi ya Kariakoo ambapo Simba ilichapwa 5-1 na ziliporudiana ikafungwa tena 2-1, huku beki huyo akitumika kwa muda mchache na kutoka akionekana kuumia kabla ya Simba kufungwa bao la kwanza.
Kiungo mshambuliaji wa Dodoma Jiji, Mghana Christian Zigah huenda msimu ujao asiwe sehemu ya kikosi hicho baada ya kumaliza mkataba.
Hakuna mazungumzo yanaendelea baina ya Dodoma na Zigah na tayari kiungo huyo wa zamani wa Biashara United aliyemaliza msimu ulioisha akifunga mabao matatu na ameondoka Dodoma akiwa safarini kurudi Ghana. Ramadhan Elias