KILELE CHA DAMU SALAMA – MICHUZI BLOG

Na Khadija Kalili , Michuzi Tv

HOSPITALI ya Rufaa Tumbi Mkoa wa Pwani imekusanya lita 300 za damu katika wiki mbili za maadhimisho ya miaka 20 ya uchangiaji damu duniani ambapo ina kauli mbiu isemayo okoa maisha changia damu.

Hayo yamesemwa leo Juni 14 na Kaimu Mganga Mkuu Kuu wa Mkoa wa Pwani Dkt. Erica Mrema katika hafla ya kilele cha maadhimisho hayo ya miaka 20 ya uchangiaji damu yaliyoadhimishwa duniani katika Hospitali ya Rufaa Tumbi ya Mkoani Pwani .

Dkt. Mrema amesema kuwa wamechangisha damu kutoka kwa makumdi mbalimbali ya vijana na akinamama wakiwemo wanafunzi kutoka Shule za Sekondari za Wilayani Kibaha na Kambi za Jeshi za Msangani na Kiluvya.

Aidha ameionya jamii kutopendelea kula chakula na chai kwani huchangia kupunguza damu mwilini.

Wakati huohuo Katibu wa Afya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tumbi Judith Mwinuka ameonya Watanzania waachane dhana potofu ya kusema wanaume waache kuchangia damu kwasababu zinapunguza nguvu za kiume na kusisitiza kuwa hii ni dhana potofu.

Amesema kuwa Mkoa wa Pwani wanamwamko hafifu katika kuchangamkia kuchangia damu hivyo elimu inahitajika zaidi.

“Uchangiaji damu una faida kubwa kwa jamii hasa kwa wagonjwa, majeruhi wa ajali za barabarani na kina mama wajawazito wakati wa kujifungua.

Naye Mratibu wa Kitengo Cha Damu salama wa Hospitali ya Rufaa Tumbi Tatu Gemela amewataka jamii kuendelea kuchangia damu maana mahitaji ni makubwa kwani hufikia Hadi lita 15 huitajika kwa siku Hospitalini hapo.

Related Posts