Akizungumza, leo Juni 14, 2024 Mkoani Iringa, Mbunge wa Njombe Mjini, Mhe. Deodatus Mwanyika, amesema nia ya kamati ya Bunge ilikuwa ni kutembele na kuona mchakato mzima wa uzalishaji wa maziwa. Na kwenye hii ziara, kamati ya Bunge imejifunza mengi na kusikiliza mafanikio na changamoto za uzalishaji maziwa. Na kuelezea kuwa wao kama washauri na wasimamizi wa serikali hii itawapelekea kujua nini hasa wafanye kwenye Tasnia ya maziwa.
Aidha Mhe. Mwanyika aliendelea kusema kwenye maziwa angalau nchi sasa inazalisha. Na nia ya kamati ya Bunge ni kulinda viwanda vya uzalishaji maziwa kwa sababu tasnia ya maziwa ina matokeo kwenye maisha ya watu kiujumla. Na kama kamati wanaangalia bajeti isiwe kikwazo kwenye sekta hii ya maziwa na ndio mana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliweka sekta hii inayojitegemea peke yake, na wao kama kamati wamelipokea hili na watatafakari.
“Ni uwekezaji mkubwa, unaofaa na unaotoa ajira. Na inakidhi kwa kila nyanja na ni vyema kuisaidia hii tasnia ya maziwa kama ina changamoto. Na kwa hiyo tunawapongeza sana Asas kwa kuzalisha maziwa bora” Mhe. Mwa yika amesema
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe, amesema mifugo nchi Tanzania inachangia asilimia 7% ya pato la Taifa, na ndani ya 7%, asilimia 30% inatokana na maziwa.
Prof. Shemdoe aliendelea kusema kuwa tasnia ya maziwa ni tasnia kubwa sana ambayo lazima ipewe kipaumbele. Nchini kuna ng’ombe wa maziwa milioni moja na tatu ambao ng’ombe hawa wanatoa maziwa lita bilioni 3.9. Lakini katika maziwa hayo bilioni 3.9, kama alivyosema Mkurugenzi Mkuu wa Asas, ni asilimia 3% tu ambayo yanakwenda kwenye biashara za viwandani, ila asilimia 97% yanauzwa mtaani kwenye chupa za Maji.
“Haya maziwa lita bilioni 3.9 tukiweka katika mfumo wa hela inatupa thamani ya shilingi Trioni 7.8 kwa mwaka. Hii ionekane ni kwa namna gani Tasnia ya maziwa inavyochangia pato la Taifa kwa hali ya juu.” Prof. Shemdoe alisema
Prof. Shemdoe aliendelea kusema Tanzania tuna viwanda jumla 152 ambavyo ni viwanda vidogo na viwanda vya kati na sita tu ndio vikubwa kimoja wapo cha Asas . Na katika hivyo viwanda 152, Asas ndio kiwanda pekee kilichoanza uzalishaji maziwa ya unga ingawa tunatumia kiasi cha Dola milioni 8.1 kuingiza maziwa ya unga kwa mwaka nchini. Japo soko tulilonalo la ndani kama tunaweza hakikisha tunazalisha maziwa ya unga kwa wingi.
“Hawa wenzetu wa Asas walivyoamua kulianza hili, sisi tuliona ni jambo jema na kubwa sana na ndio mana tunawaunga mkono” amesema Prof. Shemdoe
Akielezea mafanikio na changamoto katika uzalishaji wa maziwa katika kiwanda cha Asas, Mkurugenzi Mtendaji wa Asas, Bw.Fuad Asas, akianza na mafanikio amesema, mwaka 2000 Asas ilianza uzalishaji ikiwa na lita 1000 na wafugaji 50, lakini leo hii ipo katika uzalishaji wa lita 350,000 na wafugaji 9500 na ina wafanyakazi 400.
“Tunakusanya maziwa katika mikoa mitatu, Mbeya, Iringa na Njombe. Na tunajivunia kuwa kiwanda chenye bidhaa nyingi ambao ni mtindi, yogurt, cheese, pamoja na maziwa ya unga katika viwanda vyetu vyote viwili.” amesema Bw. Asas
Aliendelea kusema Asas wameweza kusambaza madume bora Njombe na Makambako, na kutoa elimu ya ufugaji kibiashara kwa wafugaji pamoja na kuongeza uzalishaji wa maziwa ya unga.
“Moja ya changamoto kubwa ni unywaji maziwa ni asilimia 28% tu, unywaji wa maziwa ni duni kwa sababu ya uelewa. Na hatuwezi peleka bidhaa nje ya nchi kwa sababu hakuna sera ya kuthibiti magonjwa.” amesema Bw. Asas
Picha ni sehemu ya aina ya ng’ombe wafugwao katika kiwanda cha maziwa cha Asas wakiwa katika zizi Juni 14, 2024, Iringa