UVCCM WATAKA MTANDAO WA ‘X’ UCHUKULIWE HATUA


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Nasra Ramadhan akizungumza na waandishi wa habari jijjni Dar es Salaam leo Juni 15, 2025, baada ya kukerwa na baadhi ya maudhuii ya Ngono yanayorushwa na Mtandao wa Kijamii wa ‘X’.



UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam (UVCCM), kwa kuungana na vijana wengine wa Tanzania, kutaka mtandao wa Twitter zamani kwa sasa ‘X’ uchukuliwe hatua wa kufungiwa kutokana na mtandao huo, kutumika vibaya kimahudhui kwa kuonyesha picha za ngono.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Nasra Ramadhani alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 15, 2025 hasa kupinga matumizi ya mtandao ambao umekuwa ukitoa Maudhui yake yasiyoendana na maadili ya kitanzania.


Mwenyekiti huyo ameiomba serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kulichukulia hatua za kisheria suala hilo kwa kuufungia mtandao huo, kwani ukiendelea kuwepo utaweza kuendelea kuhathiri vizazi vya sasa na vya baadae.

Aidha ameeleza kuwa ingawa viongozi mbalimbali wa dini na kiongozi wa UVCCM Taifa komredi Mohamed Kawaida kukemea suala hilo, huku baadhi ya watu na Wanasiasa mbalimbali kulichukulia suala hilo kwa kukebei, kitendo ambacho amesema siyo jambo sahihi kuendea kulifumbia macho ndani ya Taifa la Tanzania.

Related Posts