Mkuu wa Idara ya Ushauri wa Kilimo Benki ya NMB Isaack Masusu (mwenye kofia) akifafanua jambo mbele ya Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Alexander Mnyeti anayesikiliza wa kwanza kulia kwenye maonesho ya wakulima wa kisasa yanayoendelea Ubena Zomozi Halmashauri ya Chalinze Mkoani Pwani.
Na Khadija Kalili, Michuzi Blog
SHILINGI Tilioni 1.61 zimetolewa mikopo ndani ya miaka sita katika Benki ya NMB na kuwezesha ufugaji wa samaki na mazao ya chakula nchini.
Akitoa taarifa wakati wa ufunguzi wa Maonesho Jumuiya ya Wafugaji Kibiashara nchini TCCS Mkuu wa Idara ya Ushauri wa Kilimo Isaack Masusu Ubena Halmashauri ya Chalinze Mkoani Pwani amesema pia Benki hiyo imetoa mikopo ya zaidi ya shilingi Bil. 20 ambazo zimeelekezwa katika programu ya kujenga kesho iliyobora BBT.
Masusu amesema NMB kuwa inatambua changamoto ya upungufu wa mitaji ambayo hupunguza uzalishaji wa kisasa wenye tija na ndio maana wamefanya kuwezeshaji huo wa mikopo.
Amefafanua kuwa benki ya NMB imekuwa ndio benki ya kwanza nchini kuanza kutoa mikopo ya riba nafuu na tulitoa zaidi ya bilioni 100 kwa wakati huo na pesa hiyo ilitolewa kwa Wafugaji nchini.
“Lakini pia benki yetu inatoa mafunzo kwa wakulima kupitia taasisi tatu za NMB foundation, mafunzo hayo ni kwa vijana na akina mama pamoja na wafugaji kwenye maeneo yao pasipo gharama yoyote” amesema Masusu
Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Alexander Mnyeti akifungua Maonyesho hayo aliwapongeza Jumuhia ya Wafugaji kibiashara kwa kufanya Maonyesho hayo yanayoonyesha Uhalisia wa ufugaji wa kibiashara ambao utasaidia kuongea Soko la nyama ya Tanzania Kimataifa.
Tanzania ni nchi ya pili kwa mifugo barani Afrika pia tuna ng’ombe zaidi ya Mil.37.
Maonesho haya yamefunguliwa jana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Alexander Mnyeti yafungwa kesho ambapo mgeni rasmi atakuwa Naibu Waziri Mkuu Biteko.