Kamati ya kupinga ukatili wa kijinsia yalia ndoa nyingi kuvunjika na kusababisha ukatili kwa watoto.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa wananwake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) mkoa wa Njombe Scholastika Kevela ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya kupinga ukatili wa kijinsia kitaifa amewataka vijana kuwa na machaguo sahihi kabla ya kuingia kwenye ndoa ili kupunguza wimbi kubwa la ndoa kuvunjika na kusababisha ukatili mkubwa unaotokea kwa watoto.

Ametoa wito huo mjini Njombe wakati akizungumza na vijana walioko kwenye kambi maalum ambapo amesema wakati ugomvi unaendelea kwa wanafamilia na kupelekea mgawanyo wa mali hali hiyo inakwenda kuzaa ukatili kwa watoto wanaobaki kati kati.

“Wakati tunagombana na kugawana mali nusu kwa nusu hatuwaangalii watoto na ndipo ukatili unapoingia kwa kuwa mama amechukua hamsini zake na baba hamsini zake watoto wanabaki katikati hatimaye wahuni wanaamua kushughulika na ile familia”amesema Scholastika Kevela mjumbe wa kamati ya kupinga ukatili wa kijinsia kitaifa

Nao baadhi ya viongozi wa kamati hiyo mkoa wa Njombe akiwemo Shukrani Kawogo ambaye ni katibu wa siasa na uenezi wilaya ya Ludewa pamoja na Betrece Malekela ambaye pia ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Njombe wamewaomba vijana kuwa mabarozi na vipaumbele wa kutoa taarifa kwnye vyombo husika wanapoona ukatili ukitoea kwenye jamii.

“Tunataka kuhakikisha maswala ya ukatili kwenye mkoa wa Njombe hayapo,Ushoga,ubakaji wa watoto na ulawiti hayapo kwa hiyo tushirikiane kwa pamoja kwa kuwa Njombe bila ukatili inawezekana,na mkiona ukatili kwenye wilaya yako toeni taarifa bila kunyamaza”wamesema baadhi ya viongozi

Kwa upande wao vijana akiwemo Jifax Mwalongo,Kelvin Fihoma na Chariti Mkoni wameahidi kuwa mabarozi ili kutokmeza ukatili mkoani Njombe

“Sisi tunakwenda kuwa mabarozi wazuri kwa kushuka kwenye matawi na kuyazungumza maswala haya na katika mkoa wetu wa Njombe maswala ya ukatili yamekithiri sana kwa hiyo sisi vijana tunawajibu kusimama kwenye jamii na kushirikiana katika kudhibiti vitendo hivi”amesema Chariti Mkoni

Related Posts