Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa ameungana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kutoa salamu za pole kwa familia ya aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Marehemu Dkt. Shogo Mlozi tarehe 15 Juni, 2024 jijini Arusha.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa familia ya Marehemu Dkt. Shogo Mlozi tarehe 15 Juni, 2024 jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Vita Kawawa akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa familia ya Marehemu Dkt. Shogo Mlozi tarehe 15 Juni, 2024 jijini Arusha.
Balozi Mussa na Mhe. Kawawa wakimfariji Prof. Eliamani Sedoyoka ambaye ni mume wa aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Marehemu Dkt. Shogo Mlozi.
Balozi Mussa na Mhe. Kawawa wakitoa faraja kwa wazazi wa marehemu.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama walipoungana na waombolezaji wengine katika msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Marehemu Dkt. Shogo Mlozi tarehe 15 Juni, 2024 jijini Arusha.