Cheza na mwanao kama unavyocheza na simu yako, kama unvyoipenda simu yako na pia mpende mwanao kama unavyoipenda simu yako kwani ulawiti na ubakaji unafanyika majumbani, mashulei na mitaani bila kujali anasoma shule gani na ukigundua anafanyiwa ukatili chukua hatua mara moja bila kujali hata kama ni ndugu yako aliyefanya ukatili na kufanya hivyo utakuwa umewalinda watoto na vitendo vya kikatili ili kutengeneza Taifa imara lenye kumjua Mungu.
Hayo yamesemwa Juni 16, 2024 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Theopista Mallya alipokuwa akizungumza na waumini wa Kanisa la Anglican DCT lililopo eneo
la Chadulu Dodoma na kuwataka kuongea na watoto ili kuweza kubaini changamoto za ukatili wanazokumbana nazo na kuweza kuzitolea taarifa.
Katika hatua nyingine Kamanda Mallya amekemea suala la ushoga na usagaji huku akinukuu vifungu vya biblia Mwanzo 1:28, Walawi 18:22 na Warumi I 24 vinavyokataza masuala hayo kwani hata sheri za nchi zinakataza pia masuala ya ushoga na usagaji hivyo kuendelea kushabikia vitendo hivyo ni kumkosea mwenyezi Mungu na sheria za nchi.
Aidha Kamanda Mallya amewasihi waumini hao kujiepusha na mikopo ya kausha damu na Vikoba yanayosababisha madeni yaliyopitiliza na kuwataka kukopa kiasi unachoweza kulipa huku akirejea kwenye kitabu cha Zaburi 37: 21 kimeelezea kuhusiana na madeni kwani dawa ya madeni ni kulipa huku akikemea vitendo vya rushwa ambaye ni adui wa haki na hata kitabu cha Zaburi 15:5 na Kutoka 10:17 na 23:8 kinakataza kutoa na kupoekea rushwa ambayo hugeuza ukweli kuwa uongo.
Toka Dawati la Habari Polisi Dodoma.