WALIMU WALIOGUSHI UHAMISHO KUCHUKULIWA HATUA

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI (Elimu) Dkt. Charles Msonde ametoa muda wa siku moja kwa maofisa Elimu wa mikoa kuwasilisha majina ya Maofisa Elimu na walimu wanaodaiwa kugushi nyaraka za uhamisho wa vituo vya kazi ili hatua za kinidhamu zichukuliwe.

Dkt. Msonde ametoa maekezo hayo mkoani Tabora wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha kutathmini utekeleaji wa shughuli za Elimu katika robo ya pili ya mwaka cha Maofisa Elimu wa Mikoa na Halmashauri za Tanzania Bara uliofanyika katika ukumbi wa Isike Mwanakiyungi uliopo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

“Hakuna tuliyemteuwa kuanzia Julai 2022 hadi leo kwa kufanya hivyo tutapata waliokuja huko kwenu feki tunataka majina yao na walipotoka na kwasababu mnao kule barua zao wapige ‘copy’ watuletee (kesho) kwasababu hatuwezi tukakomesha hiyo tabia ‘if we don’t act now’ tutachezewa sana na inabidi sasa twende ‘beyond’ ikiwa ni pamoja na kuwafungulia mashtaka” Amesema

Akisisitiza jambo hilo Dkt. Msonde amesema jambo la kugushi nyaraka halifanyiki kwa viongozi pekee kwani mpaka sasa limefika kwenye uhamisho wa walimu “zipo Halmashauri kwa sasa zina-suffer kwasababu watu wake wamehama kwa watu walewale wanaosaini barua sasa lazima tukomeshe hiyo tabia tunataka wale wrote walioletewa barua za kuhama ambao unawasiwasi na barua zao na majina yao ili tukomeshe na tuwarudishe wote walikotoka”

Katika hatua nyingine Dkt. Msonde amewataka Maofisa Elimu wa Mikoa na Halmashauri nchini kulinda hadhi ya mwalimu ikiwemo kulipa madai yao ya madaraja na fedha za likizo ili kuwafanya walimu hao kuwa na ari na marari katika ufundishaji.

Related Posts