MBUNGE UMMY MWALIMU AUNGANA NA TAASISI YA SHITTA KUTOA SADAKA WAGONJWA BOMBO HOSPITALI KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA KUCHINJA



MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu aungana na Umoja wa Taasisi za Kiislamu Mkoani Tanga (SHITTA) kutoa sadaka kwa wagonjwa waliolazwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga (Bombo) kusherehekea sikukuu ya Eid Al_Adha kwa ajili ya kuchinja.

Mbunge Ummy alisema kwamba kushiriki kwa pamoja kutoa chakula kwa wagonjwa, kwenye Hospital hiyo ikiwa ni sehemu ya kusherehekea sikukuu ya Eid Al Adha kutawawezesha wagonjwa nao waweze kufurahia siku hiyo

Akiwa Hospitalini hapo Mbunge Ummy alionyesha furaha yake kutambulishwa shirikisho hilo ambalo linaziunganisha Taasisi za dini ya kiislamu katika mkoa wa Tanga huku akiwatoa wito kwa taasisi nyengine kuona umuhimu wa kutoa sadaka kwa wahitaji ikiwemo wagonjwa.

“Kwa kweli nimefurahi sana kushirikiana na Taasisi hii,wakati mwingine mimi kama mbunge napata shida kuzungumza na taasisi moja moja ,lakini kama nataka kukutana na taasisi za kiislamu naweza kuitafuta SHITTA ambayo inaweza kuniletea taasisi zote”,Alisema mbunge wa Jimbo hilo Ummy Mwalimu.

Related Posts