Injini ya ndege ya Australia yawaka moto ikiwa angani

Moja ya habari iliyokamata hisia za wengi kwenye mitandao ya kijamii ni pamoja na ndege ya Virgin Australia Boeing 737-800 iliyokuwa ikielekea Melbourne kutua kwa dharura  huko New Zealand baada ya moto kulipuka kutoka kwenye injini muda mfupi baada ya kupaa kutoka Queenstown.

Tukio hilo linaloshukiwa kusababishwa na shambulio la ndege aliyenasa kwenye injini , lilinaswa kwenye video ikionyesha ndege hiyo ikianza kuteketea kwa moto afisa mkuu wa operesheni wa shirika hilo la ndege, Stuart Aggs, alisema katika taarifa iliyotumwa kwa barua pepe.

Ndege aina ya Boeing 737-800 iliyokuwa na abiria 67 na wafanyakazi sita waliokuwemo ndani ya ndege hiyo ilitua katika mji wa Invercargill wa New Zealand baada ya tukio la moto kwenye ndege kulazimika kuchepuka.

“Kwa bahati nzuri, hakuna majeraha yaliyoripotiwa.

Abiria walishuka mara moja huko Invercargill na Virgin Australia walipanga ndege mpya kwa safari yao  kuendelea, huduma ya zima moto ya taifa ilisema.

Inasemekana kiwango cha ndege wanaogonga ndege katika viwanja vya ndege vya New Zealand ni takriban nne katika kila safari 10,000 za ndege, kulingana na tovuti ya udhibiti wa anga ya nchi hiyo.

 

Related Posts