Samia aeleza alivyomsitiri kaka yake kwa kutolipwa mishahara, ataka waajiri kulipa wafanyakazi

RAIS Samia Suluhu Hassan ametoboa siri namna alivyomsitiri kaka yake kwa kumlipia kodi, usafiri na matumizi mengine kwa muda wa zaidi ya miezi saba kutokana na kutolipwa mshahara na mwajiri wake kwenye chombo kimoja cha habari. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kutokana na hali hiyo ameagiza waajiri na wamiliki wote wa vyombo vya habari nchini kulipa wafanyakazi wao mishahara kwa sababu hata Serikali imenuia kulipa madeni yote yaliyohakikiwa kabla ya tarehe 24 Disemba mwaka huu.

Rais Samia ametoa maagizo hayo leo Jumanne jijini Dar es Salaam wakati akifungua kongamano la pili la maendeleo ya sekta ya habari.

“Nina mfano wa kaka yangu mwenyewe alikuwa anafanya kazi kwenye chombo kimoja cha habari lakini kodi ya nyumba nalipa mimi, matumizi nalipa mimi, usafiri wake nampa mimi… nikastahimili miezi sita hadi saba, nikamuuliza wewe hupewi mshahara au unaharibu fedha?, akaniambia hatujalipwa. Nikatafuta wenzie nikawamuuliza hivi mnalipwa mishahara au hamlipwi, wakasema Suluhu kasema kweli hatulipwi..

“Nikamuambia sikiliza, hebu toka huko njoo huku, nikamrudisha nyumbani nikamtafutia cha kwake nikampa nikambia wewe kaa hapa sasa angalia…,” ameeleza Rais Samia.

Amesema kwa upande wake atakwenda kutoa msukumo kwa wizara ya fedha ihakiki madeni hayo ili yalipwe.

Hata hivyo, amesema yapo madeni mengi ambayo hayana ushahidi kutokana na wamiliki wake kutokuwa na taaluma ya bioashara hivyo kupewa matangazo bila kufuata taratibu za kibiashara hali iliyowawia vigumu kuwa na ushahidi wa madeni yao kwa serikali.

Amesema yapo yanayolipa kwa sababu yapo mengine hayana ushahidi hivyo yatashindikana kulipwa.

Aidha, ametoa wito kwa waajiri na wamiliki wa vyombo hivyo kulipa madeni ya wafanyakazi wao wakishalipwa madeni hayo.

Related Posts