Tanzania yazindua Ujenzi wa Majengo pacha Nairobi

Serikali ya Tanzania imezindua rasmi ujenzi wa majengo pacha jijini Nairobi, Kenya yatakayotumika kama ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini humo na kitega uchumi ambapo hafla hiyo imehudhuriwa na Waziri Mkuu wa Kenya, Musalia Mudavadi.

 

Ujenzi huo utafadhiliwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF na kujengwa katika eneo la kibiashara katikati ya jiji la Nairobi kwenye eneo ambalo serikali ya Kenya iliipa Tanzania kwa ajili ya kujenga ofisa zake za ubalozi.

Akizungumza katika tukio la uzinduzi huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba, alisema mradi huo ni sehemu ya mkakati mpya wa serikali kuhakikisha inatumia maeneo na majengo yake yaliyo ughaibuni kuingiza fedha za kigeni badala ya kutumia fedha za kigeni.

Alisema mkakati wa serikali unataka kuiondoa Tanzania kutoka kutumia kiasi cha shilingi bilioni 29 kwa mwaka kulipa kodi kwenye balozi zake ughaibuni na badala yake kuingiza kiasi cha shilingi bilioni 36 kwa mwaka kama mapato ya uwekezaji kama huo wa Kenya.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Walemavu), Deo Ndejembi, alisema mradi huo umefanyika baada ya upembuzi yakinifu wa kina uliofanywa na kubainisha faida itakayopatikana baada ya kukamilika kwa ujenzi huo.

Related Posts