Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imeibuka kinara katika utoaji wa taarifa kwa umma kupitia tathimini iliyofanya na Wizara ya Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa kuangalia namna Wizara, Taasisi, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoa taarifa kwa umma kwa kipindi cha mwaka 2023/24.
Matokeo ya Tathmini hiyo yametangazwa Katika Kongamano la pili la Maendeleo ya Sekta ya Habari linaloendelea Jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Alitangaza matokeo hayo Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Thobias Makoba amesema Ofisi ya Rais – TAMISEMI imeibuka kinara kati ya Wizara 25 za Tanzania Bara katika utoaji wa taarifa kwa umma,ikifuatiwa na Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi huku nafasi ya tatu ikiwa ni Wizara ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.
Vilevile Kwa upande wa Mikoa iliyofanya vizuri katika utoaji wa Habari Mkoa wa Dar es salaam umeshika nafasi ya kwanza ukifuatiwa na Mkoa wa Mwanza huku mkoa wa Arusha ukishika nafasi ya tatu .
Pia kwa upande wa Halmashauri zilizofanya vizuri, amesema Halmashauri 20 zimefanya vizuri katika utoaji wa taarifa kwa umma ikiongozwa na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ikifuatiwa na Ilemela huku nafasi ya tatu ikishikwa na Halmashauri ya Sia.
Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mbali na maelekezo mbalimbali aliyoyatoa wakati wa hotoba, ameipongeza Ofisi ya Rais – TAMISEMI kupitia Halmashauri zilizofanya vizuri ambapo amehimiza utoaji wa Habari uwafikie wananchi wa eneo husika “tumieni vyombo vya Habari vya maeneo husika ili wananchi wapate kusikia habari za maeneo yao.