TANESCO DODOMA YATOA SEMINA KWA MADIWANI NA WENYEVITI WA MITAA

AFISA Uhusiano Huduma kwa wateja TANESCO Mkoa wa Dodoma Bi.Monica Mabada,akitoa elimu wakati wa semina ya  Madiwani kutoka katika kata za Mkoa wa Dodoma pamoja na baadhi ya kata kutoka Mkoa wa Singida na wenyeviti wa Mitaa kwa lengo la kutoa elimu kuhusu ulinzi wa miundombinu ya umeme katika maeneo yao iliyoandaliwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma.

AFISA Usalama wa TANESCO Mkoa wa Dodoma Bw.Madega Dudu,akitoa elimu kuhusu uharibifu wa miundombinu ya kusafirisha na kusambazia umeme wakati wa semina ya  Madiwani kutoka katika kata za Mkoa wa Dodoma pamoja na baadhi ya kata kutoka Mkoa wa Singida na wenyeviti wa Mitaa kwa lengo la kutoa elimu kuhusu ulinzi wa miundombinu ya umeme katika maeneo yao iliyoandaliwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma.

Akizungumza kwa niaba ya RPC Mkoa wa Dodoma SP Adonia Pumpuni,wakati wa semina ya  Madiwani kutoka katika kata za Mkoa wa Dodoma pamoja na baadhi ya kata kutoka Mkoa wa Singida na wenyeviti wa Mitaa kwa lengo la kutoa elimu kuhusu ulinzi wa miundombinu ya umeme katika maeneo yao iliyoandaliwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma.

MHANDISI Idara ya Usafirishaji Umeme Dodoma Mhandisi Philemon Tirukaizile,akizungumza wakati wa semina ya  Madiwani kutoka katika kata za Mkoa wa Dodoma pamoja na baadhi ya kata kutoka Mkoa wa Singida na wenyeviti wa Mitaa kwa lengo la kutoa elimu kuhusu ulinzi wa miundombinu ya umeme katika maeneo yao iliyoandaliwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma.

DIWANI Kata ya Manyoni Bw.Simon Mpunda,akichangia Mada wakati wa semina ya  Madiwani kutoka katika kata za Mkoa wa Dodoma pamoja na baadhi ya kata kutoka Mkoa wa Singida na wenyeviti wa Mitaa kwa lengo la kutoa elimu kuhusu ulinzi wa miundombinu ya umeme katika maeneo yao iliyoandaliwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma.

DIWANI Kata ya Zuzu Mhe.Awadh Abdallah,akichangia mada wakati wa semina ya  Madiwani kutoka katika kata za Mkoa wa Dodoma pamoja na baadhi ya kata kutoka Mkoa wa Singida na wenyeviti wa Mitaa kwa lengo la kutoa elimu kuhusu ulinzi wa miundombinu ya umeme katika maeneo yao iliyoandaliwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma.

MWENYEKITI wa Mtaa wa Chidachi Kata ya Mkoze,akichangia mada wakati wa semina ya  Madiwani kutoka katika kata za Mkoa wa Dodoma pamoja na baadhi ya kata kutoka Mkoa wa Singida na wenyeviti wa Mitaa kwa lengo la kutoa elimu kuhusu ulinzi wa miundombinu ya umeme katika maeneo yao iliyoandaliwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma.

AFISA Uhusiano Huduma kwa wateja TANESCO Mkoa wa Dodoma Bi.Monica Mabada,akitoa elimu wakati wa semina ya  Madiwani kutoka katika kata za Mkoa wa Dodoma pamoja na baadhi ya kata kutoka Mkoa wa Singida na wenyeviti wa Mitaa kwa lengo la kutoa elimu kuhusu ulinzi wa miundombinu ya umeme katika maeneo yao iliyoandaliwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakifatilia semina ya  Madiwani kutoka katika kata za Mkoa wa Dodoma pamoja na baadhi ya kata kutoka Mkoa wa Singida na wenyeviti wa Mitaa kwa lengo la kutoa elimu kuhusu ulinzi wa miundombinu ya umeme katika maeneo yao iliyoandaliwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma.

Na Gideon Gregory, Dodoma.

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma limekutana na Madiwani kutoka katika Kata za Mkoa wa Dodoma pamoja na baadhi ya kata kutoka Mkoa wa Singida na wenyeviti wa mitaa kwa lengo la kutoa elimu kuhusu ulinzi wa miundombinu ya umeme katika maeneo yao.

Akizungumza na Viongozi hao  Jijini Dodoma Afisa usalama wa Mkoa TANESCO mkoa wa Dodoma Bw. Madega Dudu amesema kwasasa maeneo mengi katika mkoa wa Dodoma yamethiri vitendo vya uharibifu wa miundombinu ya umeme jambo linaloisababishia Serikali hasara kubwa.

Amesem kupindi cha mvua wanapata changamoto kubwa kwani radi ikipiga husababisha Transfoma kuungua kutokana na kutokuwepo kwa nyaya za shaba ambazo kazi yake kubwa ni kwaajili ya ulinzi wa Transfoma hiyo.

“Kwa pamoja tunapaswa kuilinda hii miundombinu inatojengwa na Serikali kwa ghalama kubwa, pia eneo jingine la kulinda ni kwenye upande wa nyaya za shaba ambazo zenyewe kazi yake kubwa ni kulinda transfoma kwahiyo hizi nyaya ni muhimu ili kuhakikisha kifaa hiki hakipati madhara na tuendelee kujihakikishia upatikanaji wa uhakika wa umeme”, amesema.

Bw. Madega ameongeza kuwa viongozi hao ndio wenye dhamana kubwa ya kuhakikisha miundombinu hiyo ya umeme inakuwa salama pia na wananchi kuhakikisha wanakuwa walinzi wa mali hizo.

Kwa upande wa Afisa Uhusiano na Huduma kwa wateja TANESCO mkoa wa Dodoma Bi. Monica Mabada amewakumbusha kuwa endapo watakuwa na changamoto za kiufundi wasisite kutoa taarifa kupitia namba za dharura ambazo zimewekwa kuliko kukimbilia kwenye magrupu ya Whatsapp ambapo mwisho wa siku wanashindwa kutatuliwa changamoto zao kwa wakati.

“Kama unapata changamoto ambayo ni ya dharura na unataka uweze kupata msaada kwa uharaka zaidi ni vyema upige hizo namba zetu dharura kwasababu ukikimbilia kuandika kwenye magrupu hayo utatumia mwingi kulalamika bila kupatiwa ufumbuzi wa tatizo lako”, amesema.

Amesema kwasasa wanao mfumo maalum ambao mteja akitoa taarifa inapewa tiketi ambayo inamsaidia fundi kupata taarifa kwa uharaka zaidi na kuweza kumfikia mteja kwa wakati.

Pia amewakumbusha viongozi hao kuwa na utaratibu wa kukagua mifumo ya umeme kwenye ofisi zao ili kuepusha matatizo ya umeme ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara pamoja na kuangalia aina ya vifaa wanavyovitumia na uwezo wake.

Akizungumza kwa niaba ya RPC wa Mkoa SP Adonia Pumpuni amesema matukio mengi ya uharibifu wa miundombinu yamekuwa na athari mtambuka hivyo ni wajibu wa kila mtu kuwa mlinzi wa mali hizo kwani sio kazi ya mtu mmoja kuilinda hivyo ni suala la uzaIendo linahitajika katika kukabiliana na uharibifu huo unaoendelea katika baadhi ya maeno.

“Wanaofanya uharibifu huu tunawajua na tunaishi nao kwa maana hiyo kuna uwezekano mkubwa tunawafahamu, sasa kama tunawafahamu kwanini tusichukue hatua na kuna mtu hapa kachangia kuwa kwanini tusifanye sheria ya TANESCO isilingane na sheria nyingine za uhujumu uchumi kwahiyo kuna mahali kwenye usimamizi wa rasilimali za taifa panakuwa na udhaifu katika usimamizi wa miundombinu au sheria”,amesema.

Related Posts