TETESI ZA USAJILI BONGO: Ibenge kuitibulia Simba SC kwa Pokou

KLABU ya Al Hilal ya Sudan imeingilia kati dili la kiungo Serge Pokou wa ASEC Mimosas ya Ivory Coast ambaye pia amekuwa akiwindwa na Simba.

Vigogo hao wamedhamiria kufanya usajili wa maana katika dirisha hili la usajili kwa ajili ya kujiimarisha na michuano ya kimataifa msimu ujao.

Simba ipo kwenye mazungumzo na beki wa kati wa ASEC Mimosas, Antony Tra Bi Tra (25) ili kuziba pengo la Henock Inonga anayetajwa uondoka ndani ya klabu hiyo.

Inonga amebakiza mwaka mmoja kuitumikia Simba amehudumu kwenye timu hiyo kwa misimu miwili ameisaidia Simba kucheza hatua ya robo fainali Caf.

Mshambuliaji Yusuph Mhilu,  milango ipo wazi kurejea katika timu yake ya zamani Kagera Sugar, baada ya kushuka daraja na  Geita Gold msimu ulioisha.

Taarifa za chini ya kapeti, zinaeleza uongozi wa Kagera, umeacha milango wazi kwa Mhilu, endapo akihitaji kurejea ndani ya timu hiyo awe huru muda wote.

Mshambuliaji Yusuph Mhilu,  milango ipo wazi kurejea katika timu yake ya zamani Kagera Sugar, baada ya kushuka daraja na  Geita Gold msimu ulioisha.

Taarifa za chini ya kapeti, zinaeleza uongozi wa Kagera, umeacha milango wazi kwa Mhilu, endapo akihitaji kurejea ndani ya timu hiyo awe huru muda wote.

BAADA ya kuibakiza Tabora United ambayo imecheza mechi za playoff dhidi ya Biashara United, kiungo Daudi Milandu anatajwa kujiunga na Dodoma Jiji.

Dodoma Jiji ipo kwenye hatua za mwisho kukamilisha dili hilo licha ya timu yake kusalia kwa kushinda mabao 2-0 nyumbani baada ya ugenini kukubali kichapo cha bao 1-0.

Ihefu FC ipo kwenye hatua za mwisho kunasa saini ya kiungo wa FC Lupopo, raia wa DR Congo, Harvy Ossete (24) kwaajili ya kuongeza nguvu kikosini mwao.

Ihefu ambayo itanolewa na aliyekuwa kocha wa wa Simba, Patrick Aussems ‘Uchebe’ imefikia kwenye hatua nzuri ya kumalizana na kiungo huyo mshambuliaji muda owote atatambulishwa.

TAARIFA kutoka ndani ya Azam FC, zinaeleza kiungo wa kati, Adolf Mtesigwa ameongezewa mkataba wa miaka miwili ya  kuitumikia klabu hiyo, yenye makao yake makuu Chamazi, jijini Dar es Salaam.

Kulikuwa na tetesi za mchezaji huyo kutakiwa na Yanga, iliyovutiwa na kiwango chake alichokionyesha msimu ulioisha.

Related Posts