Rais Dr Mwinyi akutana na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi UAE

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amepongeza uhusiano mzuri uliopo baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hasa Zanzibar na Umoja wa Nchi ya Falme za Kiarabu-UAE.

Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo leo Ikulu Zanzibar alipokutana na Mhe.Ali Rashid Alnuaimi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi ya UAE.

Rais Dk.Mwinyi amefurahishwa na wawekezaji wanaounga mkono miradi mbalimbali Zanzibar wakiwemo Wafanyabiashara kutoka UAE.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amemweleza Mhe.Alnuaimi kuwashajihisha Wawekezaji zaidi kuja kuwekeza nchini.

Related Posts