Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
Mkurugenzi wa mawasiliano na Mfumo wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Japhet Boazi amesema kupitia mpango wa kusaidia kaya maskini wanajivunia maboresho makubwa kwa Wananchi waliopitiwa na mpango huo kwa hali zao kuboreka zaidi.
Aidha Mkurugenzi huyo amesema Tasaf imekuwa ikisaidia kaya maskini kwa kuwapa mitaji na mafunzo mbalimbali kama ya ujasiriamali na wanapofanikiwa kusimama wenyewe wanawaacha wajitegemee. katika wiki hii ya utumishi wamejipanga kuhakikisha wanajenga uelewa kwa Wananchi tofauti tofauti.
Boazi amesema hayo leo Juni 19/20224 katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi Nchini yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma.
“Wiki hii ni fursa nzuri kwetu ya kufikisha ujumbe na wale wote wenye malalamiko tutawasikiliza na kuzipatia ufumbuzi”, amesema Boazi.
“ Hapa tupo kwa ajili ya Wananchi wote wenye kutaka kujua mfuko huu unavyofanya kazi lakini pia wenye changamoto mbali mbali tutazitatua kwa kadri tuwezavyo”. amesema Boazi
Hata hivyo Mkurugenzi huyo amesema mpango wa TASAF umeleta mabadiliko mengi sana katika jamii, na inawanufaka wengi walio nufaika na mfuko huo.
Naye mmoja wa Nufaika wa wa mfuko huo Kuruthumu Abdallah amesema mfuko huo umemfungulia njia katika kufikia malengo yake ambayo alitamani kufikia.
“TASAF imenipa elimu lakini baada ya elimu walinipatia mtaji wa kuanzisha biashara yangu mwenyewe ambapo mpaka leo hii najitegemea katika kufanya biashara zangu mimi mwenyewe”,amesema Kuruthumu
“Hata hivyo TASAF imeniunganisha na Wajasiriamali tofauti tofauti na leo hii nimekutana na wenzangu katika wiki hii ya utumishi tukishirikiana lakini pia kupata ujuzi mwingine kutoka kwa wenzangu” amesema Kuruthumu.
Amewataka Wananchi wa Dodoma na vitongoji vyake kufika katika Wiki ya Utumishi wa Umma katika banda la Tasaf ili wapate taarifa mbalimbali muhimu kuhusu mfuko huo unavyofanya kazi.
Mkurugenzi wa mawasiliano na Mfumo wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Japhet Boazi akizungumza katika maonesho ya Wiki ya Utumishi ya Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma
.
Waziri wa Inchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. George Simbachawene akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la Tasaf katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika katika Viwanj vya Chinangali Park Jijini Dodoma.
Wanufaika wa mpango wa kusaidia kaya maskini unaofanywa na Tasaf katika maenmeo mbalimbali hapa nchini, wakionesha bidhaa zao walizotengeneza baada ya kupayiwa mafunzo ya Ujasiriamali na kupewa mitaji ya kuanzishia biashara.