WAKAZI MBARALI WAISHUKURU SERIKALI UJENZI MABIRIKA YA KUNYWESHEA MIFUGO,VISIMA

Na Mwandishi Wetu

WAKAZI wa Kijiji cha Manienga Kata ya Mawindi Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya ambao wanaojishughulisha na ufugaji pamoja na Kilimo wameishukuru serikali kwa kuwajengea mabirika ya kunyweshea mifugo pamoja na visima ambavyo vinawasaidia kupata huduma ya Maji safi na salama kwa sasa.

Akizungumza kuhusu mradi huo Mwenyekiti wa Kijiji cha Manienga Laison Mbende amesema kwa sasa mifugo inapata sehemu nzuri ya kunywea maji na wanaendesha kilimo vema mara baada ya vyanzo vya maji kurekebishwa.

Ambapo baada ya kumaliza kuyatumia maji hayo kutoka Mto Kyoga huyaelekeza kwenda kwenye Mto Ruaha Mkuu kwa ajili ya Ikolojia ya Hifadhi ya Taifa Ruaha.

“Tunaishuku Serikali ya awamu ya sita chini Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu fedha za mradi wa REGROW kuletwa kuchimba visima, kurejesha mikondo ya mito iliyokuwa imeziba ambapo kwa sasa tunapata maji ya uhakika.

“Pia kutujengea mabirika ya kunyweshea mifugo Maji ambayo yanatusaidia sana katika kitongoji chetu cha Chabegenja,”amesema Mbende.

Aidha wananchi hao wameahidi kuitunza miundombinu hiyo ili fedha zilizowekezwa kukamilisha ujenzi wa Mabirika pamoja na uboreshaji vyanzo vya Maji katika mito iliyokuwa imepoteza kingo zake una kuwa na tija kwao na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Ofisa Maji kidakio cha Mto Great Ruaha Abisai Chilunda ameeleza kupitia mradi wa REGROW wameweza kupanda miti takribani laki Moja na Sabini ambayo ni rafiki katika vyanzo vya maji, ujenzi wa mabirika matano ya kunyweshea mifugo yenye thamani ya Sh.milioni 570.

Pia urejeshaji mito iliyopoteza mikondo ili kutiririsha Maji katika Mto Ruaha Mkuu kwa ajili ya uendelezaji hifadhi ya Taifa Ruaha ambapo Mto Mambi umegharimu Sh. miloni 20O kwa kutumia mitambo iliyonunuliwa na Mradi wa REGROW.

Amesema mitambo hiyo iliyonunuliwa na Mradi wa REGROW uimesaidia kuokoa kias cha Sh.bilioni 1.6 kama kazi hiyo ingefanywa na Kampuni nyingine.

Aidha kupitia Mradi wa REGROW ujenzi wa Ofisi 10 za Jumuia za watumia katika Wilaya za Mufindi, Makete Mbarali na Wanging’ombe Ujenzi wake unaendelea utakaogharimu Sh.milioni 600.




Related Posts