MABONDIA wa Ngumi za Kulipwa Tanzania, Jesca Mfinanga na Egine Kayange, wameondoka asubuhi ya leo kuelekea Afrika Kusini.
Wakiwa Afrika Kusini, Jesca anatarajia kucheza pambano kuu la kuwania Mkanda wa Ubingwa wa Afrika dhidi ya Simangele Hadebe raia wa nchi hiyo.
Kwa upande wa Egine, atapanda ulingoni katika pambano la utangulizi dhidi ya Monica Mukandla kutoka Zimbabwe.
Mapambano hayo yanatarajiwa kupigwa Juni 22, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Klip Livierbeg Creation Centre huko Afrika Kusini.