BRELA YAWEKA WAZI VIWANGO VYA ADA USAJILI WA KAMPUNI

WAKALA wa wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA) wamezitaja ada za usajili wa kampuni mpya ambapo gharama zake zinaanzia Sh.20,000, Sh.1000,000, Sh.5,000,000,Sh.20,000,000 mpaka Sh.50,000,000 na kwamba viwango hivyo ni kutokana na mtaji wa kampuni husika na kwa usajili wa kampuni za kigeni gharama za usajili ni Dola za Marekani 1,190,Filing fee ni Sh.66,000 na Stamp Duty 6,200.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 20,2024 mkoani Morogoro wakati akitoa mada inayohusu usajili wa Kampuni kwa waandishi wa habari wa biashara wanaoendelea na kujengewa uwezo kuhusu majukumu ya BRELA ,Mkuu wa Sehemu ya Kampuni kutoka Kurugenzi ya Kampuni na Majina ya Biashara wa Wakala huo Lameck Nyangi amesema pamoja na mambo mengine mtu kaunzia mmoja au wa wawili ambao wanataka kusajili kampuni yao wanatakiwa kuwa na taarifa za msingi ambazo wanatakiwa kujaza katika fomu.

Amesema ili kusajili kampuni pia unapaswa uwe na akaunti pamoja na nywila ili kuingia katika mfumo wa BRELA kufanya usajili na kusisitiza katika usajili huo lazima kuwepo na taarifa muhimu za wakurugenzi kwa maana ya namba zao za NIDA na TIN No lakini pia lazima kuwe na adresi kama ni mmoja au zaidi .

“Kama ni wageni wa nje lazima uwe na hati ya kusafiria lakini lazima kuwepo na jina la kampuni na jina lenyewe lisifanane na lingine, lisiwe la matusi. lisiwe na uhusiano na majina ya Serikali.Lakini kubwa katika kampuni lazima uwe na Katiba pamoja na muongozo au muongozo wa kampuni

Aidha amesema Sheria ya usajili wa kampuni katika kifungu cha nne mpaka cha tisa kimeeleza namna gani mkataba wa kampuni au kanuni za uendeshaji unatakiwa kuandaliwa. Hata hivyo taratibu za usajili wa kampuni , kuna mabadiliko yaliyotokea ambayo yalisababisha matumizi ya mtandao na BRELA kuanzia mwaka mwaka 2018 ilitambulisha mfumo wa kusajili kampuni kwa njia ya mtandao.

Pamoja na hayo Nyangi amesema usajili wa kampuni unafanyika kwa mujibu wa Sheria ya Kampuni ya Tanzania ya mwaka 2002 ambayo ilikuwa haina tofauti na Sheria ya 1932 ambayo chimbuko lake ni Sheria ya Kingereza ya mwaka 1929.

“Lakini wengine wanasema chimbuko halisi la sheria imetokana na kampuni za India mwaka 1913 lakini sheria zote mbili zinamchango mkubwa kwa sheria ya kampuni ya Tanzania ya mwaka 1932.Kuna mfanano wa vifungu vingi ambavyo vimeletwa katika sheria ya kampuni nchini Tanzania.

“Baada ya kufika mwaka 1932 tulipoamua kuwa na Sheria za kusimamia kampuni na kuendeleza kampuni sheria yetu ilione ichukue vifungu vya sheria zile za Kingereza.Kwa hiyo uhalisia wa chimbuko la Sherie za kampuni imeanza mwaka 1929 na mwaka 1932 ndio tukaja na sheria ya kampuni sura namba 212.

“Lakini Sheria ya mwaka 1932 ilfutwa na sheria ya mwaka 2002 kwa maana ilitengezwa sheria mpya ya kampuni. Na hivyo kuwa na sheria mpya na ikabaki na sura ile ile ya 212 lakini sheria hii bahati mbaya ilipitishwa na Rais na kuanza kutumika mwaka 2006.Kwa hiyo pamoja na sheria kutungwa katika kipindi cha miaka sita iliendelea kutumika sheria ya mwaka 1932,”amesema.









Related Posts