Hawa ndio wakali wa kutupia pointi 3

UKITAKA kuwabana mafundi wa kufunga mitupo ya pointi tatu (three pointer) ili wasifunge, inakupasa ucheze nao kwa karibu muda wote wa mchezo.

Kucheza naye kwa karibu kutawafanya wachezaji hao washindwe kurusha mpira katika maeneo yao ya mitupo ya pointi tatu-tatu.

Kitakachotokea baada ya kubanwa, watupiaji hao wataishia kulalamika kuwa wanatendewa madhambi.

Tukio hilo la kubanwa kwa wachezaji hao liliwahi kumtokea mchezaji Felix Luhamba wa timu ya JKT aliyekuwa na wakati mgumu kufunga three pointer baada ya kubanwa na mchezaji Cornelius Mgaza wa timu ya Savio.

Katika mchezo huo Savio ilishinda kwa pointi 69-54.

Kwa wachezaji wanaofunga ‘three pointer’ kirahisi, ni wale wanaobaki peke yao bila ya kufuatwa na kuzongwa na mpinzani yeyote.

Hiyo ilitokea kwa baadhi ya michezo ya ligi ya BDL ukiwemo mchezo wa UDSM Outsiders na Pazi,  JKT na Ukonga Kings.

Katika mchezo wa Pazi na UDSM, wachezaji wa timu ya Pazi walishindwa kumbana Tryone Endrew na kumwacha peke yake, hali iliyofanya afunge ‘three pointer’ kiraisi bila ya kusumbuliwa.

Katika mchezo huo Outsiders ilishinda kwa pointi 71-52.

Mchezo mwingine wa Ukonga Kings na JKT, wachezaji wa timu ya Ukonga Kings walishindwa kuwabana mafundi watatu wa mitupo ya aina hiyo Baraka Sadiki, Jonas Mushi na Ferix Luhamba .

Kushindwa kuwabana huko kulifanya wachezaji hao wafunge ‘three pointer’ nyingi bila ya kubanwa, hali iliyofanya JKT iweze kuibuka na ushindi wa pointi 108-68.

Related Posts