KAMA ulikuwa unadhani beki mkongwe wa Kagera Sugar, David Luhende anajiandaa kutundika daluga pole yako, kwani kwa sasa jamaa ameingia kwenye anga la Dodoma Jiji inayomtaka kumsajili.
Uongozi wa Dodoma Jiji, umedaiwa kuanza mazungumzo na beki huyo wa zamani wa Yanga ili aitumikie kwa msimu ujao.
Luhende aliyewahi kukipiga Mwadui, Mtibwa Sugar na Yanga, amemaliza mkataba na Kagera Sugar aliyodumu nayo tangu 2018, jambo lililowafanya viongozi wa Dodoma Jiji kuanza kumsaka ili akatumie uzoefu alionao kuibeba timu hiyo iliyoyumba msimu uliopita kabla ya kuzinduka mwishoni.