MSONDE AWATAKA WALIMU KUONGEZA JUHUDI KUFUNDISHA DARASA LA TATU NA KIDATO CHA KWANZA

Naibu Katibu, Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Dkt. Charles Msonde amewataka walimu kote nchini kuongeza juhudi ya ufundishaji darasa la tatu kwa shule za msingi na kidato cha kwanza kwa shule za Sekondari kwani madarasa hayo hujenga ujuzi na umahiri wa mwanafunzi hasa kwa masomo ya lugha.

Dkt. Msonde amesisitiza hilo katika kikao kazi kati ya walimu,walimu wakuu,wakuu wa shule na wasimamizi wa Elimu wa Halmashauri mbili za Bunda DC na Bunda TC kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Bunda mkoa wa mara.

“Kama tunakubaliana kuwa tunapofundisha mtoto tunarekebisha makosa ya waliyokutangulia wanaweza wasipate ‘A’ lakini hakuna ‘F’ na ukiona ‘F’ zinapatikana jiulize wapi ulikosea kwasababu ‘F’ ni ya kwako ‘ticha’ kwasababu tulifundishwa wakati wa kufundisha popote pale usifundishe kwanza unatakiwa kuangaliwa uwezo wa mtoto,angalia utayari wa watoto, najua walimu mkiamua mnaweza mkafanya makubwa mkasaidiana na Mheshiwa Rais kuleta Mapinduzi na Mabadiliko makubwa katika elimu yetu kwasababu ninyi nyote ni wasaidizi wa Mheshimiwa Rais” amesema

Dkt. Msonde amewaomba walimu kubadilika na kuacha mazoea ili kujenga msingi mzuri wa ujuzi na umahiri kwa wanafunzi.

Dkt. Msonde yupo mkoa wa Mara kwaajili ya ziara ya kikazi ambapo anatarajia kudhuru katika Halmashauri zote za mkoa huo na kuzungumza na walimu,wakuu wa shule,walimu wakuu,maofisa Elimu na wasimamizi wa masuala ya Elimu ngazi ya Halmashauri na mkoa.

 

Related Posts