Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi akifungua kitambaa kuashiria ufunguzi wa Skuli ya Sekondari Hassan Khamis Hafidh ikiwa ni shamrashamra za kutimiza miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,kushoto ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Lela Muhamed Mussa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Skuli ya sekondari Hassan Khamis Hafidh ikiwa ni shamrashamra za kutimiza miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,kushoto ni waziri wa Elimu na mafunzo ya amali mhe.Lela Muhamed Mussa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Khamis Abdalla Said kuhusiana na vifaa vya kisasa vya kujifunzia vilivyopo katika Skuli ya Sekondari ya Hassan Khamis Hafidh ambayo ameifungua rasmi katika shamrashamra za kutimiza miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,huko Munduli Wilaya ya Magharibi “A”.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi akifurahia jambo wakati alipotembelea madarasa ya Skuli ya Sekondari Hassan Khamis Hafidh mara baada ya kuifungua katika shamrashamra za kutimiza miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi akihutubia mara baada ya kufungua Skuli ya Sekondari ya Hassan Khamis Hafidh ikiwa ni shamrashamra za kutimiza miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Sehemu ya wanafunzi na Vijana wa hamasa wa chama cha Mapinduzi wakifuatilia sherehe ya ufunguzi wa Skuli ya sekondari ya Hassan Khamis Hafidh ikiwa ni shamrashamra za kutimiza miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, huko Munduli Wilaya ya Magharibi “A”.
Wanafunzi wa Skuli ya Mtopepe wakifanya igizo la ngonjera katika ufunguzi wa Skuli ya Sekondari Hassan Khamis Hafidh ikiwa ni shamrashamra za kutimiza miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, huko Munduli Wilaya ya Magharibi “A”.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi wa jimbo la Welezo Mhe. Hassan Khamis Hafidh (kulia), Mbunge wa jimbo hilo Mhe Maulid Saleh Ali pamoja na baadhi ya wanafunzi wa skuli ya Sekondari Mtopepo alipotembelea madarasa ya Skuli ya Sekondari Hassan Khamis Hafidh mara baada ya kuifungua ikiwa ni shamrashamra za kutimiza miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR
Na Khadija Khamis – Maelezo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Husein Ali Mwinyi amesema ujenzi wa miundombinu ya skuli ina lengo la kuimarisha elimu nchini na kupunguza idadi kubwa ya wanafunzi katika madarasa .
Ameyasema hayo wakati wa Ufunguzi wa Jengo la Skuli Hassan Khamis Khafith ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzanzia huko Munduli, Uwanja wa Matebwe Wilaya ya Magharibi ‘A’.
Amesema ujenzi huo ni utaweza kuboresha kiwango cha elimu na kupunguza msongamano mkubwa wa wanafunzi katika madarasa ili kufikia idadi ya wanafunzi wasizidi 45 katika kila darasa na kuongeza ufaulu kwa kuleta matokeo mazuri kwa wanafunzi hao .
“Tunataka kuboresha kiwango cha elimu nchni na kupunguza msongano mkubwa katika madarasa, leo tunaambiwa tunataka kufikia wanafunzi wasiozidi 45 katika kila darasa ili kuongeza ufaulu mzuri pamoja na kuondosha wanafunzi kuingia mikondo miwili”, alieleza Dkt. Mwinyi.
Dkt Mwinyi amesema serikali itaajiri walimu wapya katika fani ya sayansi na hesabati ili kupunguza uhaba wa walimu sambambana maslahi ya walimu .
Aidha Rais Mwinyi aliipongeza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali pamoja na uongozi wake kwa kutekeleza vyema Ilani ya Chama cha Mapinduzi na kuvuka kiwango katika sekta hiyo ya elimu.
Pia amewapongeza walimu wa skuli ya Mtopepo ambao waliweza kustahamili katika mazingira magumu kwa muda mrefu bila ya kukata tamaa na sasa kupata faraja na kuwataka kuendelea na juhudi zao hizo .
Nae Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar leila Mohamed Salum amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Husein Ali Mwinyi kwa kuendelea kuuenzi na kuutunza Muungano.
Hata hivyo ameiahidi serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kusimamia kwa ufanisi miradi yote inayotekelezwa na kusimamiwa na wizara hiyo .
Akitoa maelezo ya kitaalamu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali .Khamis Abdalla Said amesema Skuli ya Hassan Khamis Khafith imejengwa na Kampuni ya ujenzi wa Chuo cha Mafunzo cha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kusimamiwa na kitengo cha majenzi cha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar na kugharimu jumla ya shilingi Tshs Bilioni 5,468,474,484,83/- kutoka Serikalini .
Amesema Skuli hiyo ina ghorofa tatu Madarasa 42, Ofisi ya Mwalimu Mkuu Ofisi nne za Walimu, vyoo 52. Ukumbi mmoja wa mitihani, Maabara 2, Chumba cha Tehama Maktaba moja na Stoo 4 .
Katibu huyo amewaomba wananchi wa Mtopepo kushirikiana pamoja kulitunza jengo hilo ili liweze kudumu kwa muda mrefu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.