DKT.DIMWA: DK.MWINYI AMEWASHIKA PABAYA ACT-WAZALENDO

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa, akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Jumbi katika ziara ya Wajumbe wa Sektetarieti ya Kamati Maalum ya NEC CCM Taifa Zanzibar.

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa,akivishwa sikafu na Vijana wa Hamasa baada ya kuwasili katika Ofisi za CCM Mkoa wa Magharibi iliyopo Mwera kwa ajili ya ziara ya Wajumbe wa Sektetarieti ya Kamati Maalum ya NEC ya CCM Taifa Zanzibar iliyoanza leo katika Wilaya ya Dimani Kichama.

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa,akisalimiana na Wafanyabiashara mbalimbali katika Soko la Jumbi katika ziara yake ya Wajumbe wa Sektetarieti.

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa, akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Jumbi katika ziara ya Wajumbe wa Sektetarieti ya Kamati Maalum ya NEC CCM Taifa Zanzibar. 

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa,akishiriki ujenzi wa Tawi la CCM Kisakasaka Wilaya ya Dimani Kichama.

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa,amesema viongozi wa Chama Cha ACT-Wazalendo wamekuwa wakitoa kauli za kumtukana Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi kutokana na kuwashika pabaya kwa kumaliza ajenda zao kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati akizungumza na Wanachama wa CCM wa Tawi la Fuoni Kiembeni katika ziara ya Wajumbe wa Sektetarieti ya Kamati Maalum ya NEC  CCM Taifa Zanzibar iliyoanza leo katika Mkoa wa Magharibi katika Wilaya ya Dimani Kichama Zanzibar.

Dkt.Dimwa, alisema kasi hiyo ya Dk.Mwinyi ya kutekeleza ahadi alizoa katika kampeni za uchaguzi mkuu wa dola uliopita umekuwa ni pigo kubwa kwa Chama ACT-Wazalendo kwani wamekosa ajenda na hoja za kuwaaminisha wafuasi wao na badala yake wameanzisha mtindo wa upotoshaji na porojo zisizokuwa na muelekeo kisiasa.

Katika maelezo yake Dkt.Dimwa, amewambia wanachama hao kuwa CCM ipo imara na kelele na porojo za wapinzani haziwezi kuitoa Katika malengo yake ya msingi ya kutatua kwa wakati changamoto zinazowakabili  wananchi mijini na vijijini.

Aliwasihi Wanachama wa CCM pamoja na Wananchi kwa ujumla kuendelea kukiamini Chama kwa kukipigia kura nyingi katika Uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025 ili kiendelee kuongoza dola na kufanya mambo mengi ya maendeleo yenye tija kwa vizazi vya Sasa na vijavyo.

” Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi kwa maneno ya siku hizi ameupiga mwingi tena tunasema tatu bila kwa upinzani amekuwa ni mwiba ndio maana wanatapa tapa hawana ajenda wala hoja hivyo wanaamua kupotosha na kubeza kila jambo jema linalofanywa na Serikali zetu.

Wito wangu kwenu endeleeni kutuamini na kutuunga mkono kuna mengi mazuri ya nakuja kwani CCM ni Chama chenye Viongozi wangwana na wenye utu, tumejipanga vizuri kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na maisha bora.”,alisema Dkt.Dimwa.

Alisema CCM ina dhamira ya kuimarisha Ofisi zake kuwa za kisasa ili ziendane na hadhi ya Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake.
Alifafanua kuwa Chama hicho kitaendelea kufanya siasa za kistaarabu sambamba na kuheshimu misingi ya demokrasia ndani na nje ya taasisi hiyo kisiasa.

Kupitia ziara hiyo awasisitiza Wanachama hao kuendelea kulipa ada ili Chama kipate mapato yatakayosaidia katika kutekeleza shughuli mbalimbali za kisiasa.

Pamoja na hayo aliwataka Wanachama na Wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa awamu ya pili ili wapate uhalali wa kukipigia kura katika Uchaguzi mkuu ujao.

Dkt.Dimwa akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Jumbi, alisema Serikali imejenga masoko hayo ya kisasa ili kuwawekea Wananchi mazingira bora ya kufanya biashara kwa ajili ya kuongeza vipato vyao.

Alisema baada ya masoko hayo kuanza kufanya kazi  Serikali imejipanga  kusimamia zoezi la utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu kwa wafanyabiashara na wajasiriamali ili kuhakikisha wanaendelea kuimarika kiuchumi.

Kupitia ziara hiyo Dkt.Dimwa,aliwapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi kwa utekelezaji mzuri na wenye viwango wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya Wananchi katika ziara hiyo wamepongeza kazi kubwa ya utatuzi wa changamoto za wananchi mijini na vijijini.

Akizungumza Mkaazi wa Fuoni Kiembeni Kassim Juma Bakari,alisema Serikali imeweka miundombinu bora ya maji na barabara za ndani zenye lami jambo ambalo ni kielelezo cha utekelezaji wa sera zake kwa vitendo.

Naye Khadija Abdi Kombo mkaazi wa Kisakasa, alisema maendeleo yaliyotekelezwa na Dkt.Mwinyi kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita ndio kibali cha Wananchi kuendelea kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi.

Katika ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu huyo Dkt.Dimwa amefuatana na Wajumbe mbalimbali wa kamati hiyo wakiwemo wakuu wa idara za CCM Zanzibar pamoja na manaibu makatibu wakuu wa Jumuiya zote za Chama Zanzibar.

Related Posts