Kiongozi mbio za mwenge atoa maagizo haya kwa viongozi

Katika kuendelea kuboresha utendaji Kazi Kwa Viongozi wa taasisi za serikali Kiongozi wa Mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2024 Godfrey Mnzava amewataka kutekeleza takwa la Kisheria matumizi ya Mfumo wa manunuzi kidigitali kwenye utekelezaji wa Miradi pamoja na utoaji zabuni kwenye maeneo yao, kuepusha mianya ya rushwa pia uwazi wa mchakato wa zabuni kwa wafanyabiashara wanao omba tenda serikalini.

Mnzava ametoa msisitizo huo, baada ya Mwenge wa Uhuru kutembelea na kuzindua mradi wa Ujenzi wa Box Karavati katika barabara ya Mamboya-Masombawe Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro kurahisisha usafiri na usafirishaji kuunganisha wakazi wa kata ya Mamboya na barabara kuu ya Morogoro-Dodoma.Mnzava amesema ni Lazima viongozi wa Serikali kufuata utaratibu wa Serikali kupitia mfumo Mfumo maalum wakati wa utoaji zabuni Kwa wakandarasi kuepuka lawama na upendele na kuondoa vitendo vya rushwa

Anasema kumekua na tabia ya baadhi Yao kufanya mambo kinyume na utaratibu wa kiserikali jambo ambalo limekua likileta changamoto ya utendaji Kazi Kwa wakandarasi

Awali akisoma risala Kwa kiongozi wa Mbio za mwenge wa uhuru kitaifa meneja wa TARURA Wilaya ya Kilosa Mhandisi Juliana Lyimo amesema mradi huo umegharimu Shilingi milioni 356.

Amesema kukamilika Kwa mradi huo utakua mkombozi Kwa wakazi wa kata hiyo na kata jirani ambazo zinakumbana na adha ya usafiri Kwa miaka mingi katika kusafirisha mzigo.

Zaidi ya Shilingi Milioni 356 zimetumika kufanikisha mradi huo, utekelezaji wake ulilenga kuondoa changamoto ya muda mrefu, ugumu wa usafiri na usafirishaji wa mazao hasa kipindi cha Mvua.

Kwa Upande wake.mbunge wa Jimbo la kilosa Prof. Palamagamba Kabudi na mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya miungano wa Tanzania kwa kuendelea kutoa fedha kutelekeza miradi mbalimbali ya maendeleo

Katika wilaya ya Kilosa Mwenge wa Uhuru umetembelea jumla ya Miradi saba yenya thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 2.

Related Posts