DMI YASHIRIKI SIKU YA MABAHARIA DUNIANI

CHUO Cha Bahari Dar es Salaam ( DMI) kimeshiriki katika maonyesho ya siku ya mabaharia Duniani ambayo Kitaifa yanaadhimishwa katika viwanja vya Nia Njema vilivyopo katika Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Maonesho hayo yaliyoandaliwa na Wizara ya Uchukuzi yamehusisha taasisi mbalimbali za serikali na wadau wa tasnia ya bahari yameanza Leo tarehe 22-25/06/2024 na yamefunguliwa na Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohamed, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Lengo la maadhimisho hayo ni kutambua mchango unaotolewa na mabaharia duniani na kitaifa hususani katika nyanja za kibiashara, uchumi na jamii kwa ujumla.










Related Posts