TANZANIA Prisons Queens imesema mechi mbili zilizobaki katika ligi ya mabingwa wa Mikoa kwa soka la Wanawake wanahitaji ushindi tu ili kujihakikishia kupanda daraja.
Ligi hiyo ambayo inafanyika jijini Dodoma, Maafande hao katika mechi mbili walizocheza wameshinda mmoja dhidi ya Zabibu Queens 2-1 na kupoteza 3-1 kwa Katoro Queens na kuwa nafasi ya pili.
“Mechi zilizobaki kundi letu C dhidi ya Young Stars na Singida Rising Stars, tunahitaji pointi sita, vijana wako fiti na tayari kupambana” alisema Kocha Mkuu wa timu hiyo, Laurent Malambi.