Uswisi wafuzu baada ya kutoka sare na Ujerumani – DW – 24.06.2024

24 Juni 2024

Katika mechi za Kombe la EURO 2024, jana usiku Ujerumani ambao wameshafuzu hatua ya mtoano, walilazimishwa sare ya 1-1 na Uswisi ambao pia matokeo hayo yamewawezesha kusonga mbele.

https://p.dw.com/p/4hPoM

Euro 2024 Ujerumani yalazimishwa sare ya 1-1 na Uswisi
Mchezaji wa Ujerumani Jamal Musiala (kushoto) akijaribu kudhibiti mpira na kumzuia mchezaji wa Uswisi Remo Freuler wakati wa mechi yao mjini Frankfurt: 23.06.2024Picha: Michael Probst/AP Photo/picture alliance

Katika mechi nyingine, Hungary waliicharaza Scotland katika dakika za nyongeza bao 1-0. Wakiwa na pointi tatu na tofauti ya mabao, Hungary sasa watalazimika kusubiri ili kujua iwapo watafika hatua ya mtoano.

Soma pia: Shirika la reli la Ujerumani linanufaika kwa ongezeka la abiria katika kipindi hiki cha Euro 2024

Leo Jumatatu, Albania watashuka dimbani na Uhispania, huku Croatia wakimenyana na Italia.

 

Related Posts