Na Janeth Raphael MichuziTv – Bungeni Dodoma
Mbunge wa Kilosa Profesa Palamagamba Kabudi ameishauri Serikali kuwekeza katika Mkoa wa Morogoro ambao unaweza kusukuma uchumi wa Nchi kwa kuwekeza katika nishati ya maji katika Mabwawa yote Matatu ya Kihansi, Kidatu na Bwawa la Mwalimu Nyerere.
Mbunge huyo ametoa kauli hiyo Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia hoja katika hotuba ya bajeti kuu ya serikali.
Ameeleza kwamba Mkoa Morogroro unaweza kuchangia zaidi uchumi wa nchi kwa sababu wilaya ya Kilosa ni kuiunganishi ya reli tatu, reli ya SGR, reli ya Tazara na reli ya kati.
“Ukiangalia pembe tatu ya Kimamba, Kilosa na Ilonga ndio maeneo makubwa yenye utafiti mkubwa wa kilimo, hivyo ukijenga reli mpya kutoka Mkata stesheni kwenda Dumila na kuboresha Mkata stesheni kuwa ndio kituo kikubwa cha machinjio ya ng’ombe ili nyama hiyo ije Dar es salaam kupitia SGR na Kiwanja cha Msalato kwenda Nje,” alisema Palamagamba
Tukiwekeza katika Mikoa Michache na kufanya ndio nguvu ya kusukuma uchumi nchi itapiga hatua kubwa, na nina Imani kubwa na Wizara ya Mipango pamoja na Tume ya Mipango na niko tayari kukaa naoi li kuja na mpango mkakati wa maendeleo wa wilaya ya kilosa na Mkoa wa Morogoro.