Serikali kuendelea kushirikiana na viongozi wa dini

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema serikali inaendelea kushirikiana na viongozi wa dini kuhakikisha suala la maadili nchini.

Jana, Chalamila alikua mgeni rasmi akimwakikisha Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, katika Ibada ya Maadhimisho ya Miaka 90 ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Albano, Upanga jijini Dar es Salaam.

Alilitaka kanisa hilo kuendelea kujitafakari katika maadhimisho hayo kwa namna wanavyochangia maadili mema katika jamii.

Pia, amewataka waumini kuendelea kuiombea jamii kuishi katika maadili mema huku akisema serikali itashiriki katika upatikaji wa mahitaji mbalimbali ya Kanisa hilo.

Alisema kuwa Rais Dk.Samia kukubali mwaliko huo, sio jambo jepesi hivyo ni kazi kubwa na heshima kubwa waliyompatia Rais Dk.Samia hivyo kumtuma amuwakilishe.

Alisisitiza suala la maadili kwa kuhakikisha kanisa linasisitiza maadili kwa waumini kuepuka vitendo hivyo.

Alisema haipendezi kuona baadhi ya viongozi wa dini kupata kashfa kwa matendo yasiyo na maadili ikiwemo masuala ya ulawiti na mauaji ya watu wenye ulemavu wa albaino.

Alisema kuwa kanisa linaonwa kama kimbilio na msaada kwa jamii hivyo waendelee kutekeleza imani hiyo na kuepukana na matendo ya malumbano na migogoro.

Alisema kuwa ni kanisa ambalo limetunza mambo mengi sana hivyo serikali inaliona ni sehemu yake kwa umuhimu wake huo.

Aliwapongeza kwa kazi kubwa na jitihada za kuendeleza katika hilo hadi kuanzisha miradi ya kanisa hilo ikiwa ni hatua kubwa ya maendeleo na kutunza maadili nchini huku akisema wataendelea kushirikana nalo kwa ukaribu.

“Miaka 90 sio jambo la kawaida, ni kubwa hivyo serikali wanaungana nao katika maadhimisho hayo ya miaka 90 ya kanisa hilo, 

Kuhusu kampeni ya Kuondoa wadada wanaojiuza

Alisema kuwa kwa lengo la kuendeleza kazi nzuri inayofanywa na kanisa ya kuhakikisha jamii inakuwa salama na kuepukana matendo hayo yasiyo na maadili katika jamii.

Alieleza kuwa mambo hayo sio mazuri hivyo sio jambo la jamii kuyatetea na kuyashabikia.

Kasisi Mkuu wa Kanisa Kuuu Jacob Kahemele aliishukuru serikali kwa namna ambavyo wanaendelea kupata huduma nzuri kupitia viongozi wa serikali ambao wamekuwa wakitenda haki.

Walimpongeza Rais Dk.Samia kwa namna ambavyo ameendelea kuliongoza Taifa kwa kuwepo amani na upendo nchini.

Alisema kuwa wamekuwa wakiwahudumia wahitaji mbalimbali wakiwemo yatima na kufanya matembelezi mbalimbali yanayolenga kuhudumia jamii.

Alisema wanaujenzi wa mradi mkubwa wa uwekezaji, unaendelea kutekelezwa kupitia michango mbalimbali ya waumi hao.

Katibu Mtendaji wa Dayosisis ya Dar es Salaam, Lameck Ndomba aliwapongeza kanisa hilo Kwa maadhimisho hayo huku akiwaomba fedha zitakazopatikana kuendelea kusaidia makundi mbalimbali na kuzingatia maono ya kanisa.

Aliwashukuru viongozi wa serikali walioudhuria wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam huku akisema kuwa wanaendelea kumuombea katika kuendelea kutekeleza majukumu yake,

Akielezea historia ya Kanisa hilo, Mbunge Profesa Palamagamba Kabudi, ambaye ni muumini wa Kanisa hilo, alisema ni muhimu kutunza historia ya Kanisa hilo kwa kudumisha umoja na amani zaidi na sio kuendeleza mabishano ya tofauti.

Alisema kanisa hilo linamapokeo mengi zaidi ya 20, huku akiwataka kudumisha mapokeo hayo kwa msingi wa amani na upendo

Alisisitiza kuendelea kutunza mambo yanayofanana kuliko kubishana kwa yale yasiyofanana

Alieleza kuwa, Neno Anglikana ni la Kilatini lililoanzishaa nchini Uingereza kama kikundi cha uamsho na baadaye kuanzishwa Marekani likiwa na msingi wa kutokulazimisha mambo.

Alisema ni kanisa Moja Takatifu linalotunza maagizo ya mitume likiwa na madaraja makuu mawili maaskofu na mashemasi huku akisema sio kanisa pekee lenye mapokeo zaidi ya moja.

Alisema Kanisa la Anglikana lilifika nchini eneo la Tanga Karne ya 19 kupitia umishionari ambapo kwa eneo la Pwani na Dar es Salaam, lilifuata baadaye na maeneo mengine katika kuanzisha kanisa hilo.


Related Posts