RC PWANI AHIMIZA MAENDELEO ZAIDI MJI WA KIBAHA

 

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akizungumza  kwenye kikao hicho

Baadhi ya Madiwani  walishiriki kwenye kikao hicho.

Mwenyekiti  wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mussa Ndomba  akifafanua jambo.

Na Khadija Kalili , Michuzi Tv

MKUU wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge ametoa wito kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha kutobweteka na hati safi ya makusanyo waliyoipata na kushika nafasi ya tatu ndani ya Mkoa wa Pwani .

RC Kunenge amesema hayo leo Juni 24 katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji Kibaha amewataka kutoridhika na ushindi huo wa hati safi na kuwasisitiza waende mbali zaidi ya sifa hiyo.

Kunenge amesisitiza Halmashauri wazingatie maagizo ya Kamati za Bunge ambayo imekemea kumalizika kwa jengo la Halmashauri ya Mji Kibaha ambalo halijalamilika kwa muda mrefu nasisitiza ikibidi chinjeni kondoo, mbuzi iteni masheikh mapadri waje wakemee ili jengo hili liweze kukamilika hii ndiyo taswira ya Mji wa Kibaha lakini mtu akipita hapaeleweki hivi ni nani aliyeturoga Pwani?

Mkuu huyo wa Mkoa ametoa rai hiyo mbele ya viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi Mwenyekiti wa CCM Wilaya Kibaha Mwl.Mwajuma Nyamka, Mkaguzi Mkuu wa Mkoa Pwani Pastory Massawe, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon, Kamati ya Ulinzi na Usalama, Madiwani wa Wilaya ya Kibaha pamoja na Viongozi kutoka katika Idara mbalimbali za Halmashauri ya Kibaha .

“Tuna wajibu wa kuujenga Mji wa Kibaha na uwe na taswira ya kuvutia kwa sababu hivi sasa mkiulizwa Mji wa Kibaha uko wapi hakuna majibu yoyote mtakayo nipa hivyo nawahimiza viongozi wote kwa pamoja tutekeleze maelekezo yaliyotolewa na Kamati ya Bunge kuwa kuna umuhimu wa kuijenga Kibaha na kuachana mapori ambayo yametuzunguka pia kwa wale wawekezaji wote ambao wamepewa maeneo yaliyo kwenye uso wa mji lakini wameshindwa kuyaendeleza wanyang’anywe”amesema RC Kunenge.

Nawa sisitiza suala la kuupanga mji kwa anayetaka kujenga kwenye uso wa mji atimuliwe mji uwe na sura ya kuvutia mbele ya watu pindi wanapoingia Kibaha.

Aidha kuhusu Halmashauri ya Mji Kibaha kuibuka na hati safi amesema kuwa anawapongeza katika ukusanyaji wa mapato na kushika nafasi ya tatu katika ngazi ya Halmashauri za Mkoa wa Pwani ambapo ya kwanza ni Chalinze Bil.15.6 ikifuatiwa na Mkuranga Bil.13 na ya tatu Kibaha Mji iliyokusanya kiasi cha Bil.7 lakini amewataka kutobweteka na kuwataka wajipange kufanya vizuri zaidi na kupandisha kiwango cha kukusanya chamapato na kuwashauri madiwani pamoja na uongozi wa Halmashauri watengeneze fursa wenyewe kwa sababu fursa huwa haimfuati mtu bali hutengenezwa.

“Katika mabaraza yetu tujipange kuzungumzia kuhusu masuala ya kukuza uchumi wa Halmashauri na lazima tuweke alama ya kudumu Kibaha Mji pindi tutakapoondoka hivyo kwa pamoja tuutengeneze mji wa Kibaha” amesema RC Kunenge.

Amesema kuwa matumizi mazuri ya mapato ni pamoja na kukusanya ni jambo moja na matumizi ni jambo lingine na kuwataka wajikite zaidi kwa kuzidisha mbinu za ukusanyaji mapato.

“Miradi ilete tija ndani ya Halmashauri na kuwe na matokeo chanya kwa wananchi ambao wanataka kuona maendeleo kama vile kufikishiwa huduma za maji,nishati ya umeme,shule , zahanati barabara nanhuduma zote muhimu zinazohitajika kwa jamii na siyo vinginevyo” amesema Kunenge.

RC Kunenge ameongeza kwa kusema kuwa ikiwa baadaye mwaka huu nchi nzima itaingia katika mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa anawaomba viongozi wote walioaminiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM ) kuhakikisha wanashinda katika kila eneo ambalo wanaliongoza na si vinginevyo.

“Wajibu wangu kama Mamisaa wa Mkoa wa Pwani ni kuhakikisha CCM inashinda katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025”.

Wakati huohuo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mussa Ndomba amesema wamekubali kupokea maelekezo yote yaliyotolewa na Mwakilishi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, ambaye ni Mkuu wa Mkoa Kunenge ikiwa ni pamojana Kihaba Mji kukosa sura halisi lakini tunaahidi tutatekeleza kwa kushirikiana na TANROAD,TARURA kwa ujenzi wa barabara kutoka Mkoani Wilayani na kuingia mitaani ikiwa ni pamoja na kuweka taa barabarani pia mamlaka zingine tutashirikiana nazo katika kuupendezesha Mji.

Related Posts