TIMU ya Tanzania Prisons imeanza usajili na tayari imemalizana na beki wa kushoto Aboubakar Ngelema, ambaye msimu ulioisha alikuwa na Dodoma Jiji.
Mwanaspoti imepata taarifa za uhakika za Ngalema kusaini miaka miwili katika kikosi hicho na muda wowote wanaweza wakamtangaza.
Chanzo cha taarifa kutoka ndani ya Prisons kimesema: “Ngelema ni mchezaji halali wa Prisons, kwani tumemsainisha mkataba wa miaka miwili kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Dodoma Jiji.”
“Ngalema ni kati ya wachezaji ambao wamependekezwa na kocha wetu mpya, Mbwana Makata ambaye pia bado hatujamtangaza.”
Alipotafutwa kuzungumzia hilo, Ngalema amesema: “Suala hilo lipo ndani ya uongozi wa Prisons siwezi kuzungumza chochote kwa sasa. Wao ndio wanapaswa kuwatangaza wachezaji wao.”