Dk Biteko mgeni rasmi kongamano la MSMEs

Dar es Salaam. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la wajasiriamali wadogo, wa chini na wa kati (MSMEs).

Kongamano hilo linaloandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communictions Limited (MCL), litafanyika Julai 5, mwaka huu, badala ya Juni 27 iliyotangazwa awali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na MCL, kongamano hilo litafanyika katika eneo litakalotangazwa baadaye, badala ya ukumbi wa The Super Dome uliokuwa umetangazwa.

Kwenye kongamano yatajadiliwa masuala mbalimbali katika kuhusu kuboresha, kuendeleza ujuzi na kukuza biashara zinazochipukia, ndogo na za kati.

Wajasiriamali na wadau wengine kutoka taasisi mbalimbali zikiwamo za fedha, wanatarajia kuhudhuria kongamano hilo.

“Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utaka  ojitokeza kutokana na kuahirishwa kwa tarehe ya awali ya kongamano hili,” imeeleza taarifa ya MCL.

Hili litakuwa kongamano la pili la wajasiriamali wadogo na wakati kuandaliwa na MCL, baada ya lililofanyika mwaka jana na kuhudhuriwa na maelfu ya wajasiriamali.

“Hii ni fursa ya kuungana na Serikali, wabunifu, wafadhili, mabenki na wataalamu wa teknolojia kujadili masuala muhimu kama vile ubunifu, fedha, ukuaji na uendelevu katika biashara zinazochipukia,” imesema taarifa.

Taarifa mbalimbali kuelekea kongamano hilo zitaendelea kutolewa kupitia magazeti ya Mwananchi na The Citizen na kurasa za mitandao ya kijamii ya Mwananchi.

Related Posts