Aliyekuwa kocha Singida BS atangazwa kumrithi Ramovic Yanga

Muda mfupi baada ya kocha Sead Ramovic kubwaga manyanga, Yanga leo, Februari 4, 2025 imetangaza kumchukua kocha wa Singida Black Stars, Hamdi Miloud kuziba pengo lililoachwa na Mjerumani huyo.

Taarifa iliyotolewa na Yanga imesema kuwa Ramovic ameondoka sambamba na msaidizi wake Mustafa Kodro.

“Uongozi wa Klabu ya Young Africans SC umefikia makubaliano ya pande mbili kuvunja mkataba na Kocha Sead Ramovic na msaidizi wake Mustafa Kodro.

“Katika hatua nyingine, Klabu ya Young Africans SC inamtangaza Kocha wake mpya, Miloud Hamdi mwenye uraia wa Algeria na Ufaransa.

“Kocha Hamdi mwenye uzoefu mkubwa wa kufundisha soka akiwa amefanya kazi

barani Ulaya, Asia na Afrika, anaungana na timu mara moja kuanza majukumu yake mapya.

“Kocha huyo mbali na uzoefu alionao, pia ana mafanikio makubwa katika soka la Afrika akishinda taji la Ligi Kuu ya Algeria na kucheza Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2015-2016 akiwa na USM Alger,” imefafanua taarifa hiyo ya Yanga.

Miloud anajiunga na Yanga akiwa ameitumikia Singida Black Stara kwa siku 37 tu huku akiwa hajawahi kuifundisha katika mechi hata moja ya mashindano.

“ Hamdi amewahi kufika hatua ya fainali katika Ligi ya Mabingwa Afrika, robo fainali mara mbili Ligi ya Mabingwa Afrika na robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Vilevile, Kocha Hamdi ana uzoefu mkubwa na Soka la Afrika kwa kuzinoa klabu mbalimbali kwa mafanikio makubwa kama vile USM Alger na JS Kabylie za Algeria, A

Related Posts