Wafanyabiashara 774 kati ya 1,520 waliotambuliwa kuwa na sifa za kurejeshwa katika soko la Kariakoo


WAFANYABIASHARA 774 kati ya 1,520 waliotambuliwa kuwa na sifa za kurejeshwa katika soko la Kariakoo wamejitokeza leo (Februari 07,2025) katika ukumbi wa mikutano wa Arnautoglo Dar es Salaam kuchukua fomu maalum za usajili kwa ajili ya maandalizi ya kuingia kwenye soko hilo kufuatia tangazo la kukamilika kwa uhakiki wa wafanyabiashara na majina kutangazwa kwa umma.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Menejimenti ya Shirika la Masoko ya Kariakoo leo imeonesha kuwa kazi ya kuchukua, kujaza na kisha kurejesha fomu hizo imeanza leo na itakamilika siku ya Ijumaa tarehe 7 Februari 2025 kisha taratibu za uchukuaji na ujazaji wa mikataba kati ya Shirika na mfanyabiashara itaendelea.
Wito unatolewa kwa wafanyabiashara wote ambao majina yao yametangazwa kutumia muda uliotolewa ili kuchukua na kujaza fomu hizo maalum hatua itakayosaidia kurahishisha utartibu wa kurejesha biashara kwenye soko la Kariakoo.
Itakumbukwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo hawa Ghasia alitangaza mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa biashara katika Soko la Kariakoo zitarejeshwa tena kuanzia mwezi huu na kwamba ifikapo Februari 22 mwaka huu zitaanza kufanyika kwa muda wa saa 24.

Related Posts